All Right Receved by MR.PENGO 2016

Friday, April 24, 2015

MKAZI WA KAWE IRENE MREMA ACHOMOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 100 ZA JAYMILLIONS.

Balozi wa Promosheni ya JayMillions Hillary Daud”Jaymillions” na Rosalynn Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,wakimshuhudia Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- Irene Mrema ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam akisoma tarakimu kwenye hundi ya fedha alizojishindia kupitia promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni hiyo, iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam Irene Mrema aliyeibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/= kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,akiwa amepozi kwenye picha na hundi yake baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia(hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Rosalynn Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania na Balozi wa Promosheni ya Jaymillions Hillary Daud”Jaymillions” wakimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, Irene Mrema(aliyeshikilia hundi) mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kukabidhiwa kitita chake. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

Mshindi mwingine wa kitita cha shilingi Milioni 100/kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Irene Mrema (30) mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam leo amekabidhiwa kitita cha fedha alizojishindia katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Vodacom Makao makuu Milima City jijini Dar es Salaam.

Irene Mrema ambaye ni Ofisa manunuzi na ugavi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mama mwenye watoto wawili amesema kuwa amefurahia ushindi huu na ana imani kitita alichojishindia kwa kiasi kikubwa kitayabadilisha maisha yake kuwa bora zaidi kwa kufungua miradi ya kujikimu kimapato na kusaidia familia yake na ndugu zake.”Nashukuru Mwenyeji Mungu kwa kuniona na nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni kwa ushindi huu nimeamini kuwa Jaymillions sio promosheni ya mzaha na matangazo bali ya ukweli na nawasihi watanzania wenzangu tuchangamkie fursa hii”.Alisema kwa furaha.

Promosheni ya Jaymillions inayoendelea ikiwa inakaribia kufikia mwisho imeishawawezesha baadhi ya wateja wa Vodacom kuwa mamilionea kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi watatu wa milioni 100/-washindi sita wa milioni 10/-na washindi 40 wa milioni 1/-na maelfu ya wateja wamejishindia muda wa maongezi.

Washindi wa milioni 100/-ni Uwezo Madegenge kutoka wilayani Kilolo mkoani Iringa , Khamis Khalid kutoka Mtwara na mshindi wa leo ni Irene Mrema wa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, amempongeza mshindi na kutangaza kuwa kutokana na maombi ya wateja promosheni hiyo imeongezewa muda wa wiki mbili zaidi hadi May 7 ili kutoa fursa kwa wateja kuendelea kujaribu bahati zao.

No comments: