Thursday, March 26, 2015

WANAWAKE JITOKEZENI KUWANIA NAFASI YA URAS- TGNP.

Mwanaharakati  wa TGNP  kutoa kijiji  cha   Ifiga kata ya Ijombe Mbeya  Bi . Flora Mathias Mlowezi akifafanua  jambo  wakati  wa mafunzo ya  wanahabari juu ya wajibu  wa  wanawake na  vijana kujitokeza katika kuwania nafasi za  uongozi
washiriki  wa  mafunzo ya  TGNP kwa  wanahabari wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakisikiliza kwa makini mada mbali mbali zilizokuwa  zikitolewa katika mafunzo  hayo
Wanahabari  wakimsilikiza Bi Mlowezi
Bi Mlowezi  akielezea jinsi alivyofungwa  jela miezi  mitatu  kutokana na kufanya harakati kijijini kwake
wanahabari  wakiwa  katika  warsha hiyo
 afisa mawasiliamo ya TGNP Bw  Melikizedeck  Karol wakati  akitoa  mada ya  uchaguzi  mkuu

Na matukiodaimaBlog, Mbeya

WAKATI  vuguvugu  la  uchaguzi  mkuu mwaka  2015  likiendelea  kushika kasi  ndani  ya  vyama vya  siasa kwa  wanachama mbali mbali  kujitokeza kutangaza  nia ,mtandao  wa  jinsia Tanzania (TGNP)  umewataka  wanawake nchini kujitokeza  kutangaza  nia ya  kuwania nafasi  ya Urais .

Wito   huo  umetolewa afisa mawasiliamo ya TGNP Bw  Melikizedeck  Karol wakati  akitoa  mada ya  ushiriki  wa   wanawake  kwenye  uchaguzi  mkuu mwaka 2015 wakati  wa mafunzo ya siku  mbili ya  wanahabari  mikoa ya  nyanda  za  juu  kusini yaliyomalizika  leo jijini Mbeya.

Alisema  kuwa  usawa  katika nafasi  za uongozi  wa  kutaka  kuwa na asilimia 50 kwa 50 kati ya  wanawake na  wanaume ni lazima  utimie  katika uchaguzi  huu  kwa  wanawake kuanza  kujitokeza kuwania nafasi  mbali mbali zikiwemo  za  juu kama Urais ,ubunge  na udiwani .

Karol  alisema  kuwa  kasi ya  wanawake na vijana  kujitokeza katika nafasi mbali mbali  za  uongozi inapaswa  kuanza  kujionyesha  kuanzia  sasa  ili  ikiwezekana bunge la baada ya  uchaguzi  mkuu 2015 idadi ya  vijana na  wanawake  iongezeke  zaidi bungeni.

"Hivi  wataka  kusema hakuna  mwanamke katika  nchi hii ambae  anaweza kuongeza nchini kama Rais na kama wapo  kwanini  hawajitokezi  kugombea nafasi za  juu kama Urais .....lazima  wanawake  wachangamkie nafasi  hiyo "

Kwani  alisema  kuwa  katika  jamii  mwanamke ndie  anayekumbwa na  changamoto  mbali mbali katika  jamii na  kuwa  iwapo  wanawake  wataendelea  kuwa  nyuma katika  kuwania nafasi  hizo bado changamoto  zilizopo  zitaendelea  kuwatesa  wanawake .

Alisema kwa mwaka 2005  kuwa akidi nzima ya  bunge la jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  ni wabunge 357 kwa  mujibu  wa katiba  hata  hivyo  viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa  kuzingatia  matokeo  ya uchaguzi kati ya  viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio  walipewa viti  vya  kuchaguliwa bungeni.

Huku  idadi  ya  madiwani  wa  kuchaguliwa  asilimia 4 na  wenyeviti wa  vijiji ni  asilimia 2 wakati  wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .

 Hivyo  alisema  ni  wajibu  kwa  vyombo  vya  habari na  wanawabari  nchini kuendelea kuhamasisha  makundi  ya  vijana na  wanawake  kujitokeza  kwa  wingi katika nafasi  za  udiwani ,ubunge na Urais katika  uchaguzi  mkuu mwaka huu.

Alisema  kuwa  sera ya Taifa ya  vijana pamoja na mkataba  wa vijana wa Afrika  unalitambua kundi la vijana kama ni  rasilimili  mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo  na  pia katika kulinda amani na utulivu kwenye bara  la afrika.

"Hata  hivyo pamoja na kwamba vijana ni  zaidi  ya asilimia 60 bado mchango na thamani ya  vijana haujulikani  ipasavyo kwenye Demokrasia ya  Tanzania  huku thamani yao  ikionekana tu nyaraka  za  uchaguzi  kwa kutumiwa kama walinzi au wapambe  wa wagombea"

Alisema  ni vema  vijana  kujitokeza  kujiandikisha katika daftari  la kudumu la  wapiga  kura ili  kuweza  kutumia haki yao  ya msingi  ya  kuchaguliwa na kuchagua .

No comments: