All Right Receved by MR.PENGO 2016

Monday, March 2, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KATIKA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA KAPTENI JOHN KOMBA,KAJIMJEE JIJINI DAR LEO.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.Picha zote na othman michuzi.
  Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiifariji familia ya marehemu.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.
 Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
Kamanda Kova.
Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
Familia ya Marehemu.
Watoto wa Marehemu Kapteni John Komba wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu baba yao.
Mjane wa Marehemu,Kapteni John Komba,Mama Salome Komba akiaga mwili wa mumewe
Khadija Kopa.
Umati wa viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba.
Post a Comment