Wednesday, February 18, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA LINDI, MTWARA.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud Kulia kwa Waziri.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Matanki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo jirani.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kushoto) akimwonyesha kitu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati alipotembelea Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, mwanzoni mwa wiki.
Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu. 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara yake kukagua Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Mhandisi Kapuulya Musomba na kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud. 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kushoto), akisalimiana na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Msimbati, Joha Matwili, alipowasili MnaziBay kujionea athari za mmonyoko wa ardhi uliotishia hali ya usalama wa mazingira ya Kampuni ya Tawel & Prom inayozalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara. 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu (aliyenyoosha mkono), akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, jinsi maji ya bahari yalivyoathiri eneola MnaziBay, karibu na kampuni ya kuzalisha umeme ya Maurel & Prom. 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (aliyenyoosha mkono) akimwonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (wa pili kulia) wakati Waziri alipotembelea eneo hilo kujionea athari za mmomonyoko wa ardsalama wa mazingira ya Kampuni ya kufua umeme ya Maurel & Prom iliyo jirani na eneo hihi uliotishia ulo. 
Athari ya mmomonyoko wa ardhi katika eneo la MnaziBay inavyoonekana pichani. Mmomonyoko huo umetishia usalama wa Kiwanda cha kufua umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara cha Maurel & Prom.
Meneja Uzalishaji na Uendeshaji wa Kampuni ya Maurel & Prom, David Chajdronnier (katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu (Kulia) kuhusu mmomonyoko wa ardhi eneo la MnaziBay, Mtwara. Kampuni hiyo ndiyo inazalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Mtwara na Lindi. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu. 
Kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara. Kisima hiki hupokea gesi asilia kutoka Kisima namba 1 na Kisima namba 2, kisha kupelekwa Madimba kwenye mtambo wa kuchakata gesi hiyo. 
Sehemu ya mtambo wa kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara ambacho hupokea gesi kutoka Visima namba 1 na 2, kisha kupelekwa Madimba katika mtambo wa kuchakata gesi. 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akicheza mchezo wa ‘Pool Table’ katika ukumbi uliopo kwenye nyumba za wafanyakazi wa mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara baada ya kuhitimisha ziara yake mwanzoni mwa wiki. Mahali hapo pa michezo ni maalum kwa wafanyakazi kwa ajili ya kujichangamsha baada ya kazi. Anayefuatilia mchezo huo ni Msaidizi wa Waziri, Mhandisi Joseph Kumburu. 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akikagua moja ya Valvu ya gesi, eneo la Somanga Fungu akiwa katika ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini na mwenye kofia nyeupe ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba.

No comments: