All Right Receved by MR.PENGO 2016

Saturday, February 28, 2015

MH. JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO.

Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari,zinaeleza kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halimashauri kuu CCM Taifa,Mh. Kaptain John Komba amefariki dunia kwenye Hospitali ya TMJ,Mikocheni jijini Dar es salaam.

Mh. Komba amefariki Dunia majira ya saa 10 jioni ya leo na mwili uko hospitalini hapo. 

Kaptain Komba alizaliwa Machi 18, 1954 wilayani Mbinga baada ya kusomea ualimu aliacha kufundisha na kujiunga na jeshi mwaka 1978, ambapo alipanda cheo hadi kufikia kaptaini na Mwaka 1992 alijiungia kitengo cha uhamasishaji cha CCM.

Katika kipindi chote hicho marehemu alikuwa mahiri katika kutunga nyimbo mbalimbali lakini zaidi ni zile za uhamasishaji kwa chama cha Mapinduzi

Mungu aiweke roho ya marehemu mahapa pema

-Amin.
Post a Comment