Tuesday, January 6, 2015

WAAMUZI 11 NCHINI TANZANIA NA NA BEJI ZA FIFA.

 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya waamuzi waliopata hadhi ya kuwa waamuzi wenye beji za FIFA katika hafla fupi ya kukabidhi Beji hizo,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Jumla ya waamuzi 11 wamepata Beji ya FIFA mwaka huu na kupelekea idadi ya waamuzi wote nchini wenye Beji hizo kufikia 18.Picha zote na Othman Michuzi wa globu ya jamii dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa akizungumza machache katika hafla hiyo.
 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akisisitiza jambo kwa waamuzi waliopata beji za FIFA wakati akiwaonyesha kitabu cha Maadili ya FIFA katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
 Kiongozi wa Waamuzi wanaume waliopata Beji ya FIFA,Mujuni Mkongo (kati) akizungumza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TFF kwa jitihada walizozionyesha mpaka kuwafanikisha wao kupata hadhi hiyo,pia alitoa wito kwa Waamuzi wengine kuipenda kazi yao na wajitume zaidi.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi na kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa.
 Kiongozi wa Waamuzi wanawake waliopata Beji ya FIFA,Hellen Mduma akizungumza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa shukrani zake kwa niaba ya Waamuzi wenzake.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi na kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Jonesia Rukyaa katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Sophia Mtongori katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Florentina Zabron katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Msaidizi Grace Muhindi katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Waamuzi waliopata Beji ya FIFA pamoja na wageni mbali mbali.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Kiongozi Mujuni Mkongo katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wamuzi Tanzania,Salim Chama.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Msaidizi, Sudi Hilla katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wamuzi Tanzania,Salim Chama.
Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi ukiwa katika picha ya pamoja na waamuzi hao waliopata Beji ya FIFA.

No comments: