Saturday, January 10, 2015

TANESCO ILIVYO SHEREHEKEA MWAKA MPYA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA CHAKUWAMA,SINZA JIJINI DAR


 Mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam akionyesha umahiri wake wa kudaka taswirazz kwa kutumia simu.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Amne Hilal akipata Selfie na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam,wakati walipowatembelea jana kusherehekea nao kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Amne Hilal akiwaonyesha picha yao watoto hao wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam
Mmoja wa watoto waliopo kwenye kituo hicho.
Mmoja wa maafisha wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Lusajo Mwakabuku akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki (mwenye shati jeupe walioketi mbele) wakati walipowatembelea na kusherehekea nao mwaka mpya 2015,watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis (aliesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu kituo hicho mbele ya uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) waliotembelea kituo hicho kwa lengo la kujumuika pamoja na watoto hao katika kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Leila Muhaji akifafanua jambo mbele Watoto Yatima wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam. 
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis (kulia) akitoa maelezo ya kituo hicho kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki wakati alipokuwa akimtembeza kwenye maeneo mbali mbali ya Kituo hicho.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Leila Muhaji.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki wakati wakiwa kwenye moja chumba cha msimamizi wa kituo hicho ambacho kipo katika hatua za mwisho kumalizika.
Amne Hilal akifurahi na Baadhi ya Watoto wa kituo hicho.
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Bibi Saida Hassan akizungumza na vyombo vya habari wakati uongozi wa Tanesco ulipotembelea kituo chake hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho,ambapo amefarijika sana kuona maendeleo ya watoto katika kituo hicho.ambapo waliweza kuwapatia watoto hao vifaa vya shule na vyakula kama sehemu ya mchango wao.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis akitoa shukrani kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kuwatembelea kituoni hapo,huku akitoa wito kwa wengine kuendelea kukitupia macho kituo hicho,kwani bado kinahitaji kusaidiwa.
Afisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Khadija Ahmed (kati) akimnyesha maziwa Mtoto Badra mwenye umri wa miezi saba (7) anayelelewa kwenye kituo hicho baada ya kutupwa na Mama yake nje ya kituo hicho akiwa na miezi mitano (5).wanaoshuhudua ni Queen Mwashinga (kulia) na  Henry Kilasila.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki akimkabidhi baadhi ya vifaa mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho ikiwa ni sehemu vifaa walivyowaletea watoto hao.
Sabuni.
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Tanesco kwa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki  akimkabidhi risiti ya Umeme Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis ikiwa ni moja ya vitu vilivyokuwa vikihitajika kituoni hapo.
Maafisa wa Tanesco,Neema Mbuja (kulia) na Amne Hilal wakiweka mambo sawa kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa kituo hicho.
Muda wa chakula ukawadai.
Picha ya pamoja.

No comments: