All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, January 11, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AWAANDALIA TAFRIJA YA MWAKA MPYA WENZA WA MABALOZI WA NJE WALIOPO TANZANIA.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal (wa kwanza kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa tarfija ya mwaka mpya aliyowaandalia wenza wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania tarehe 10.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Anna Mkapa wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nje hapa nchini.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa kwa hotuba yake na Mama Celine Mpango, Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini. Mama Mpango ni kiongozi wa wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wenza wa mabalozi na wageni waalikwa kupiga picha ya kumbukumbu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na na baadhi ya wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyowaandalia huko Ikulu tarehe 10.1.2015.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal akijadiana jambo na Kiongozi wa wenza wa mabalozi waliopo hapa nchini Mama Celine Mpango wakati wa tafrija ya mwaka mpya. PICHA NA JOHN LUKUWI.
Post a Comment