Wednesday, July 26, 2017

JUBILEE INSURANCE YAADHIMISHA MIAKA 80 KWA KUJENGA VYOO SHULE YA MSINGI ITIJI JIJINI MBEYA..


 Jubilee Insurance Katika kuadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo ya bima Imezinduwa vyoo katika shule ya  msingi Itiji iliyopo jijini mbeya vyoo hivyo vyenye jumla ya matundu 12 vilivyo jengwa na kampuni hiyo ya bima ya Jubilee Insurance na kuzinduliwa na  Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania  Consoleta Cabone baadaya ya kuguswa na changamoto ya  vyoo katika shule mbalimbali za msingi nchini.
 Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania  Consoleta Cabone akizungumza machache kati ya mengi aliyo yazungumza alisema "Naipongeza sana Jubilee Insurance kwa kujitoa kujenge vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Itiji, kwani ni jambo kubwa na linalo fanya na wacheche na badara ya kufanya sherehe kubwa katika maoteli kugawana kile kilicho baki kwenye bima na hatimae kurejeshwa kwa wananchi kwa kufanya mambo mema yenye baraka ikiwemo hili la ujenzi wa vyoo kwenye shule mbalimbali za msingi" pia Consoleta Cabone alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo yanayozungukwa na shule hiyo kulinda na kudhamini vyoo vilivyo jengwa na Jubilee Insurance.
Meneja wa Tawi la  Jubilee Insurance kwa nyanda za juu kusini ndugu, Anne Qares akisoma lisala mbele ya mgeni rasmi Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania  Consoleta Cabone katika uzinduzi na ufunguzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Itiji vyoo vilivyo jengwa na Jubilee Insurance.
 Mkuu wa Shule ya msingi Itigi Mwl Lightness E. Makundi Akitoa shukran kwa Jubilee Insurance kwa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule yake.

  Mgeni rasmi akiwa katika zoezi  la uzinduzi wa vyoo shule ya msingi Itiji iliyopo jijini mbeya.

No comments: