All Right Receved by MR.PENGO 2016

Thursday, January 12, 2017

MVUA YAWATEMBELEA WANA JIJI LA MBEYA LEO...

Kamera yetu Ilipo kuwa ikiangazia maeneo mbalimbali ya Taswira za Jiji la Mbeya leo ilijikuta ikikuibulia Taswira mbalimbali za Mvua iliyotamba kwa kitambo kuanzia asubuhi ya leo mpaka saa nane mchana na kuweka hali ya usawa kwa wanambeya hasa kwa wafanyabiashara mbalimbali Jijini Hapo Ikiwa ni muendelezo wa Mvua za Masika kama ambavyo unavyo hapo juu chombo cha usafiri aina ya Bajaji kikiwa kimetumbukia kwenye dimbwi la Maji maeneo ya Shule ya Sekondari Sinde Jijini Mbeya.
Hapa ni ndani ya uzio wa Soko kuu la kimataifa Soko la Mwanjelwa eneo la wafanya bishara ndogo ndogo maarufu kwa jina la Wamachinga wakiwa wamejiweka sawa kwa kujiongeza kufunika bidhaa zao zisiathiliwe na Mvua.
Hapo kila mtu na Mwamvuli wake mitaa ya Ilemi jijini Mbeya.
Hivi ndivyo mambo yalivyo noga leo Jijini Mbeya.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.
Post a Comment