Friday, December 16, 2016

PROF-MWANDOSYA AHUTUBIA CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)....

Mkuu wa chuo cha sayansi na teknolojia Profesa Mark Mwandosya ahutubia wanafunzi wa chuo cha sayansi na teknolojia pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa mbeya na nje ya mkoa wa mbeya. Profesa Mwandosya sambamba na uongozi wote wa chuo hicho cha sayansi na teknolojia wanafunzi na wadau mbalimbali wazungu mzia juu ya kuboresha huduma zitolewazo na  chuo hicho hasa kwa kutoa elimu kwa wanafunzi katika masomo ya sayansi na teknolojia ambapo inaonyesha idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hicho wengi ni jinsia ya kiume, Profesa mwandosya amesema kuwaidadi kubwa ya  watu wana ya kimbia masomo ya sayansi na teknolojia kwa dhana ya kuhisi masomo hayo ni magumu haswa kwa jinsia ya kike, Masomo yasayansi na teknolojia ni masomo amboyo yanamjenga mtu kiakili na kifikra pia kukupa uwezo mwanafunzi kujiajili pia kuwaajili watu,Masomo ya sayansi na teknolojia sio magumu kama ambavyo wengi wanadhani, uwezo wa kuwapata wanasayansi wazuri wenye kuweza kuwakilisha vizuri ndani na nje ya Tanzania tunao na wakati ni sasa kuwahimiza watoto wetu kuwaandaa vizuri kujifunza sayansi na teknolojia.
Profesa Mwandosya akihutubia hadhara katika hutuba aliyokuwa akiitoa kwa wanafunzi na wadau mbalimbali walio hudhuria chuoni hapo katika ukumbi wa Nyerere chuo cha Sayansi na teknolojia Mbeya mjini.
Makamu mkuu wa chuo cha sayansi na teknolojia mbeya Profesa Joseph Msambichaka akizungumza na wadau pamoja na wanafunzi wa chuo cha sayansi na teknolojia hawapo pichani.
Baadhi ya wadau na wanafunzi wan chuo cha sayansi na teknolojia walio hudhuria hutuba ya profesa Mark Mwandosya Mkuu wa chuo cha sayansi na teknolojia Mbeya.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

No comments: