All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, November 6, 2016

PENATI YAWAPA USHINDI YANGA WA GOLI 1,0 DHIDI YA TANZANIA PRISON MBEYA....

Saimon Msuva Akitimuwa Vumbi kwa shuti kali wakati akipiga penati katika lango la Tanzania Prison na kuipatia yanga goli moja kwa bila katika mchezo ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya Ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Ya Soka Vodacom Tanzania Bara.
TIMU ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya askari magereza wa mkoani Mbeya Tanzania Prisons na ku�kisha jumla ya alama 30 wakiwa nyuma ya alama tano dhdi ya Mahasimu wao wakubwa Simba ambao wamepoteza mchezo wao wa leo. Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ulikuwa wa kasi na kila upande ukicheza kwa umakini uliweza kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza huku kila timu ikiwa haijaona lango la mwenzake. Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko na kuanza kulisakama lango la Tanzania Prisons lakini makosa ya washambuliaji wa timu hiyo walishindwa kutumia nafasi hizo na kukosa magoli, lakini makosa ya mabeki wa Yanga yalisabababisha Prisons kupata penati lakini uwezo wa golikipa Beno Kakolanya aliweza kuokoa mkwaju huo. dakika ya 74 mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga anaipatia Yanga penati inayopigwa na Simon Msuva na kuiandikia Yanga goli la kuongoza na mpaka dakika 90 za kumalizika kwa mchezaji huo.
Kutoka Shoto ni Haruna Niyonzima wa Timu ya Yanga Akimuomba Radhi Mchezaji Mwenzie Wa Timu ya Yanga Saimon Msuva Pindi alipokuwa Akijibizana Na Muamuzi. 
Victor Hangaya Shoto Akimpoteza Deus Kaseke.
Kutoka Shoto ni Benjamin Asukile akichuwana Vikali na Mwinyi Haji katika mtanange wa Yanga na Tanzania Prison ulio chezwa Katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
PICHA NA MR.PENGO MAELEZO ZAINAB NYAMKA MMG.
Post a Comment