Thursday, July 28, 2016

RC MAKALLA AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWA KARIBU NA WANANCHI....

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ameendelea na utaratibu aliyojiwekea wa kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kila siku ya Alhamisi ya mwanzo wa mwezi na siku ya alhamis ya mwisho wa mwezi kama kawaida siku ya leo mamia ya wananchi wamejitokeza Mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha kero zao.
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa wilaya na watendaji wa ngazi zote kuwasikiliza wananchi na kutatua Kero zao "Kero Nyingi hapa ni za Halmashauri, Wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa Idara tafadhalini hakuna jambo kubwa katika Uongozi kama kuwa Karibu na unaowaongoza, kuwa msikivu na kushughulikia matatizo yao kwa umati huu ni dhahiri hamjatimiza majukumu yenu na kwa kuwa MaDc, ma Ded ni wapya sasa anzeni kazi hii kwa kasi "
Amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa kesi na pia kuepuka vitendo vinavyolalamikiwa kwa baadhi ya Askari kubambikizia Wananchi kesi
Amehaidi kuendeleza utaratibu huu kwa muda wote mpaka siku atakapofika ukumbini akute hakuna Mwananchi aliyeleta Kero.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiendelea kuratibu na Kuandika baadhi ya kero Sanjari na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mh.Mariam Mtunguja katika ukumbi Mdogo uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Jijini Mbeya.
Kutoka Shoto ni Mkuu wa Wilaya Ya Mbeya Mjini mh,William Mtimika, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mh.Mariam Mtunguja Wakiendelea na kazi ya kunukuu kero za wananchi walio hudhuria kuwasilisha kero zao (Hawapo Pichani).

Baadhi ya Wananchi wa wakitoa Kero Zao mbele ya Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Mh.Amos Makalla.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

No comments: