Wednesday, July 27, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AMETOA SIKU SABA KUONDOA MALORI YOTE YA MIZIGO JIJINI YANAYO PAKI KINYUME NA TARATIBU.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla ametoa siku saba kwa Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuyaondoa magari yote ya mizigo yanaya paki pembezoni mwa Barabara kuu kinyume na utaratibu wakati kuna vibao vinaeleza ni marufuku magari ya mizigo kupaki maeneo hayo." Siwezi kuendelea kuona magari yamejazana hapa kuna vibao vinakataza lakini watu hawatii matatizo hayo madiwani mpo, viongozi mpo, Takataka zinazagaa Watendaji Mpo, Viongozi Tupo kuanzia leo Usafi wa Jiji letu ni Sehemu ya kipaombele na kwa kuanzia magari yote ya mizigo ndani ya wiki moja yaondoke yapelekwe eEneo lililotengwa "

Hayo ameyasema leo katika kikao cha pamoja na madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakati wa kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Serikali  (CAG)
Kuhusu ukusanyaji wa Mapato amewataka Watendaji na Madiwani kudhibiti Mapato kwa kuhakikisha Mapato yote yanakusanywa kwa njia ya (Elektroniki) 
Aidha amewataka madiwani kukagua miradi ili miradi hiyo iliyojengwa ieandane na Thamani ya Fedha.

Baadhi ya madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakifuatilia kwa makini mkutano.
Wapili Kutoka Shoto ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Mh,Amos Makalla, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mh,Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mh,Joseph Mbilinyi (Sugu) Katika picha ya pamoja baada ya Mkutano Kumalizika.

No comments: