Wednesday, April 29, 2015

KICHUPA CHA LEO.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 50 KUTOKA KAMPUNI YA TSN NA MIPIRA 50 KUTOKA KAMPUNI YA SMART SPORTS KWA AJILI YA MASHINDANO YA KINONDONI CUP.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda 'Kaka Bonda'
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.

DKT. SHEIN AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI RUVUMA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.

Tuesday, April 28, 2015

KICHUPA CHA LEO.

MICHUZI TV NDANI YA SIMUTV JIUNGE SASA UFAIDI VINONO.

Unajua kilichojiri kwenye Danga Chee ya Michuzi TV? Fuatilia popote ulipo ukiwa na SIMU.tv. 

Kujiunga piga *149*01# chagua Shangwe, kisha SIMU.tv(MPYA) kisha Video hitajika kisha Habari kisha Michuzi TV kwa walio na laini za Vodacom. Kwa yeyote mwenye simu au tablet ya Android pata app ya SIMU.tv kwenye Google play; bofya hapa: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.SIMU.t
v.

Monday, April 27, 2015

KONGAMANO LA UHURU WA HABARI WPFD KUFANYIKA MOROGORO MEI 2-3, WADAU ZAIDI YA 200 KUSHIRIKI.

MISATAN Chairperson Simon Berege addresses the media during a press conference to introduce World Press Freedom Day 2015
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro.
TMF Director Ernest Sungura clarifies a point during the conference
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam leo. Kulia Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama.
Ms Jane Mihanji, UTPC Vice President tells why it is important for journalists to be at centre stage during celebrations
Makamu Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waancdishi wa habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akisisitiza umuhimu wa wanahabari kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Mei 2 mwaka huu. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura.
KAS's Richard Shaba and TAMWA's Godrida Jola listen to questions from journalists
Miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) Bw.Richard Shaba kutoka KAS Tanzania na Mwakilishi kutoka TAMWA, Godrida Jola wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
A cross section of journalists covering the press conference
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria mkutano huo.
Journalists at the press conference


Na Modewjiblog team
Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro  kwa siku mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani (WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu.

“Hii ni mara ya kwanza WPFD kuadhimishwa mkoani Morogoro na mwakani itafanyika mkoa mwingine nia ni kufanya kila mkoa kupata nafasi ya kuadhimisha siku hiyo. Wakati wa maadhimisho hayo wadau watakumbuka gharama za waandishi wa habari kukusanya taarifa mbalimbali na kuwapatia wananchi, gharama ambazo wakati mwingine ni uhai wao au hata kunyimwa uhuru’ alieleza Berege. Aidha siku hiyo watakumbukwa wale waliopoteza maisha kutokana na harakati za kutafuta habari kwa ajili ya umma.

Siku ya WPFD, ambayo huadhimishwa duniani kote kila mwaka ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuadhimisha kanuni za uhuru wa habari na kuwakumbuka wale waliokufa wakijaribu kutekeleza kanuni hizo. Kwa maneno mengine WPFD ni jukwaa linalotumika na waandishi wa habari na wadau wengine katika kutoa kauli za kushawishi serikali mbalimbali kutunga sheria rafiki za vyombo vya habari ambazo zitahakikisha uwapo wa uhuru wa habari.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Usalama wa habari katika ulimwenguj wa dijiti: Uandishi bora, Usawa wa jinsia na faragha’. Berege alibainisha kuwa, kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo, WPFD 2015 itaangalia masuala matatu muhimu: Ikiwemo Uandishi bora na ulio huru katika dunia ya dijiti. Humu itajadiliwa uwingi wa vyombo vya habari na athari zake katika majukumu ya uandishi na uwajibikaji kwa umma, masuala ya kujiwabisha wenyewe, changamoto katika habari za uchunguzi, kauli za uchochezi na vyombo vya habari na mafunzo ya habari.

Pia suala lingine ni juu ya Wanawake na menejimenti ya vyombo vya habari; na namna vyombo vya habari vinavyomuona mwanamke huku la mwisho likiwa ni suala la Usalama wa waandishi wa habari hasa katika maeneo yenye vurugu na jinsi ya kuhami vyanzo vya habari dhidi ya ufichuaji wa kidijiti. Katika kongamano hilo pia litatoa nafasi ya kujadili na kutoa maazimio kuhusu sheria zilizopitishwa na bunge na zile ambazo zimetamkwa kwa mara ya kwanza. Sheria hizo ni pamoja na za Cybercrime Act, Statistics Act, Media Services Bill and the Access to Information Law.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Wakati wa kongamano hilo walioathirika kwa kuvunjwa kwa uhuru wa habari watatoa ushuhuda wao. Pia taarifa ya hali ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na MISA itazinduliwa rasmi.

Aidha, katika tukio hilo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez huku wadau zaidi ya 200 wakiwemo wadau wa habari na maendeleo pamoja na wawakilishi kutoka serikalini na mashirika mbalimbali ya kimataifa, mabalozi, wabunge, vyama vya kijamii, asasi zisizokuwa za kiserikali, waandishi maveterani,wakuu wa vyuo vya habari na waandishi wa habari.

Tukio hilo limeandaliwa kwa pamoja na Media Institute of Southern Africa-Tanzania Chapter [MISA (T) Chapter], Media Council of Tanzania [MCT], Tanzania Media Fund [TMF], Union of Tanzania Press Clubs [UTPC], United Nations Tanzania Office, UNESCO.

Wengine ni Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania [KAS], Media Owners Association of Tanzania [MOAT], Tanzania Editors’ Forum [TEF], Tanzania Media Women’s Association [TAMWA), Morogoro Press Club na Tanzania Communication Regulatory Authority [TCRA).

Aidha kamati ya maandalizi ya WPFD 2015 imewezesha tukio hilo kwa kushirikisha pia Government Employees Pensions Fund [GEPF], Alliance One Tanzania, IPP Group of Companies, European Union (EU) na Tanzania National Parks [TANAPA].

KICHUPA CHA LEO.

MAKONDA AIENDELEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE SAFARI HII NI KATA YA WAZO.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwahutubia wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Juu iliyopo uliopo Kata ya Wazo Dar es Salaam jana, alipofika kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu.
 DC Makonda akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wakata ya Wazo kuhusu mgogoro huo.
  DC Makonda akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Mtaa wa Kilimahewa Juu uliopo Kata ya Wazo jijini Dar es Salaam kuzungumza na wananchi kuhusu mgogoro huo. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Frank Kalinga na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Kuruthum Kazema.
 Diwani wa Kata hiyo, John Mome akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili azungumze na wananchi.
 Ofisa Tarafa wa Kawe, Nicodemus Shirika akizungumza katika mkutano huo.
 Mkazi wa mtaa huo, Kauli Kibiriti akitoa ya moyoni kwenye mkutano kuhusu mgogoro wa ardhi.
 Bibi Rosemary Mkasa akitoa historia ya maeneo hayo ya ardhi yanayogombaniwa.
 Mkazi wa eneo hilo, Philipina Uledi naye akitoa ya moyoni kuhusu mgogoro huo.
 Wananchi wa mtaa huo wakiwa kwenye mkutano huo
 Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakishangilia wakati DC Makonda akizungumza nao ili kupata muafaka wa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/

UZINDUZI WA SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 70 YA UMOJA WA MATAIFA WAFANA JIJINI DAR

DSC_0361
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini. Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi hilo.
DSC_0372
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
DSC_0380
IMG_0162
DSC_0388
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
DSC_0396
DSC_0404
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akila kipande cha cake kwenye mnuso huo.
DSC_0407
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakilishana cake kabla ya kupata chakula cha usiku wakati wa shamra shamra za uzinduzi wa miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
DSC_0412
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
IMG_0172
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakijumuika kwenye chakula cha usiku wakati wa sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
IMG_0179
IMG_0188
IMG_0225
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifuatiwa na Afisa Habari wa UNIC, Usia Nkhoma Ledama wakipakua chakula cha jioni kwenye mnuso huo.
IMG_0190
IMG_0193
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakijisevia nyama choma ndani ya hoteli ya White Sands.
IMG_0220
IMG_0197
IMG_0202
IMG_0213
IMG_0207
IMG_0222
BAADA YA KUPATA BUFEE LA NGUVU ULIWADIA ULE WASAA WAKUFANYA DIGESTION YA CHAKULA KWA KUSAKATA RHUMBA...
IMG_0253
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakisakta rhumba kwenye hafla ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
IMG_0303
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakionyesha ufundi wa kusakata rhumba kwenye mnuso huo.
DSC_0502
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye shati ya kijivu) naye hakubaki nyuma alionyesha umahiri wake.
DSC_0493
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye alionyesha ufundi wake kama anavyoonekana pichani.
DSC_0484
Usia Nkhoma Ledama naye akasema hata wasinichezee hawa.... akajibu mapigo.
DSC_0487
Burudani ikiendelea kwa furaha na amani.
DSC_0533